Table Of ContentW  M  
asifu fupi Wa
Imam muhammad 
BIN hasaN (a.s.)
Mwandishi:
M
R D
OHAMED  AZA  UNGERSI, Ph.D.
Mtarjuma:
M
S.K
UHAMMAD    ANGU
Kimetolewa na : 
Bilal Muslim Mission of Tanzania 
S.L.P. 20033 
Dar es Salaam - Tanzania
Toleo la Kwanza: 
Sha‘ban 1434 / Juni 2013
Idadi: 
Nakala 1000
Fedha kwa ajili ya uchapishaji ilitafutwa na :
BILAL COMREHENSIVE SCHOOL
Kimetolewa na :
BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA
S.L.P 20033
DAR ES SALAAM - TANZANIA
YALIYOMO
Dibaji . . . 1
Utangulizi . . . 4
Sura 1: Imam Muhammad bin Hasan (a.s.) Al-Mahdi: 
Kuzaliwa Kwake na Maisha ya Utoto. . . . 6
Sura 2: Imam Mahdi (a.s.): Ghaibat Fupi na Ndefu (Ghaibat 
Al-Sughra na Ghaibat Al-Kubra) . . . 18
Sura 3: Filosfia ya Ghaibat . . . 31
Sura 4: Yako Wapi Makazi ya Imam Mahdi (a.s.) . . . 40 
Sura 5: Majukumu na Wajibat za Wafuasi wa Imam (a.s.) 
Wakati wa Kipindi cha Ghaibat . . . 42
Sura 6: Kujitokeza Tena kwa Imam Mahdi (a.s.) . . . 48
Sura 7: Raj’at (Marejeo) . . . 56
Sura 8: Miujiza ya Imam Mahdi (a.s.) . . . 60
Sura 9: Semi za Imam Mahdi (a.s.) . . . 63
Maswali . . . 66
DIBAJI
Hivi ndivyo ilivyoanza.
Nilipokea  barua  kutoka  kwa  Mhubiri  Mkuu  wa  Bilal  Muslim  
Mission of Tanzania, Allama Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, akiniomba 
niandike masomo ya kufundisha kwa ajili ya Masomo ya Kimataifa 
kwa njia ya Posta juu ya Historia ya Uislamu ambayo Taasisi hii 
imekusudia kuyafanya. Kuwa muwazi zaidi, jukumu langu lilikuwa 
ni kuandika Vitengo (Units) tofauti 13, katika muundo wa vijitabu,  
vikiwa  na  maelezo  mafupi  ya  wasifu  wa  maisha  ya  Hadhrat  
Fatima  (s.a.)  na  Maimam  Masoom  12.  Madhumuni  yalikuwa:  
Vijitabu  hivi  viwe  rahisi  kusomwa,  vikikusudiwa  kwa  ajili  ya 
Mashia/Waislamu  wapya  na  vijana  wa  jumuiya  ya  Waislamu, 
wanaotafuta elimu kuhusu Maimam Masoom. Allama Rizvi kwa 
makhususi alisema kwamba vijitabu hivi havikukusudiwa kwa ajili  
ya wanachuoni bali wasomaji wa kawaida na kwa hivyo lazima  
viepuke mitego ya kiusomi.
Kwangu  mimi,  ina  maana  ya  heshima  ya  pekee  na  utambuzi.  
Kwamba  Allama  Rizvi,  mmoja  wa  waandishi  na  mwanachuo 
mashuhuri  katika  ulimwengu  wa  Shia,  lazima  ameniona  mimi 
kuwa na uwezo wa kuelewa majukumu haya, ni kitu ambacho  
kamwe sijawahi kukiwazia katika ndoto zangu za kawaida! Sasa kwa 
vile fursa hii ilikuwepo pale, nilikubali changamoto hii kwa sababu 
mbili. Kwanza, hii itanipa mimi fursa adimu ya kufanyakazi chini 
ya usimamizi wa karibu wa Allama Rizvi, ambaye mwongozo wake 
utafungua maeneo makubwa ya ujuzi kwa ajili yangu katika nyanja  
muhimu za Historia ya Uislamu. Pili, nitakuwa ninafanya kazi  
ambayo inaweza kuwa sababu kwangu mimi kupata ‘SAWAB-E-
JARI’ mara tu nitakapoondoka ulimwenuni hapa kwenda Akhera.
Nilikubali tume hii. Matokeo ya mara moja yalikuwa ni kitengo  
cha  kwanza  katika  muundo  wa  kijitabu:  IMAM  ALI  (a.s.)  
kilichotoka  mwaka  wa  1992.  Kijitabu  hiki  kilitoka  baada  ya  
1
kupitiwa  na  kutathminiwa  na  Allama  Rizvi  mwenyewe.  Kwa  
baraka za Allah, kilipokelewa vizuri sana na jumuiya. Nilitiwa moyo 
na  mwanachuoni  mwinginc  mashuhuri,  Malim  Ali  Mohamed  
Jaffer wa Bilal Muslim Mission of Kenya. Alinisifia kwa kuweza  
kutoa  kijitabu  rahisi  lakini  chenye  taarifa  muhimu,  ambacho  
kinafaa kwa wale wenye haja ya kupata ujuzi kuhusu Maimam 
kutoka Familia ya Mtume (s.a.w.w.). Aidha, Malim Ali Mohamed 
Jaffer alisisitiza kwamba lazima niendelee mbele na kutoa vijitabu 
kwa ajili ya Maimam 11 waliobakia. Na nilifanya hivyo, kitengo 
kwa kitengo, katika miaka iliyofuatia.
Nilipokuja kufikiria, niliona kwamba ukamilishaji wa mradi huu 
haikuwa  safari  nyepesi  kwangu.  Jukumu  hili  lilihusisha  utafiti 
mkubwa na mpana, ukitumia muda mkubwa na nguvu. Hii ni kwa 
sababu kuandika kwa ajili ya maisha ya watu hawa mashuhuri kuna 
hitaji hadhari ya hali ya juu katika kutumia taarifa sahihi na uteuzi 
wa maneno yanayofaa. Ukiongeza juu ya hili, mradi huu ulikuwa  
katika  mfumo  wa  hiyari  na  ulikuwa  ufanywe  wakati  ambao  
nilikuwa na kazi ya kila siku kwa ajili ya kunipatia kipato cha  
kujikimu.Vipengele vyote hivi huelezea ni kwa nini imechukuwa 
muda mrefu kiasi hiki kwa mimi kukamilisha mradi huu; kitabu  
moja  kwa  wakati  kuanzia  1992-2010.  Kijitabu  cha  mwisho  
kutolewa kilikuwa juu ya maisha ya lmemu wetu wa 11 Hadhrat 
Hasan Askari (a.s.) na kilichapishwa katika mwaka wa 2001.
Baada ya kupita miaka mingi, kitabu cha mwisho juu ya maisha  
ya  Imam  Mahdi  (a.s.),  Allah  amuweke  salama  na  aharakishe  
kujitokeza kwake tena, sasa kiko mikononi mwako. Inasikitisha  
kwamba  Allama  Rizvi  hayuko  tena  nasi  leo  kushuhudia  
ukamilishaji  wa  mradi  huu.  Malim  Ali  Mohamed  Jaffer,  pia 
ameondoka  kwenye  ulimwengu  huu  wa  mpito  kuelekea  
ulimwengu wa mwisho - Akhera. Allah awalipe wanachuoni hawa 
wawili maisha ya milele ya furaha kwajuuhdi zao kwa ajili ya 
Kumtumikia Yeye.
2
Nitakuwa  sitendi  haki  kama  sitashukuru  juhudi  za  Al-Haj  
Fidahusein Hameer, mmoja wa wazee waasisi wa Bilal Muslim  
Mission  of  Tanzania.  Fidahusein  bhai  ameonesha  kiwango  
kisicho na mafano cha subira na uvumilivu katika kushughulika  
na ukawiaji wangu kuhusu ukamilishaji wa mradi huu. Hakuna 
ambaye angeweza kuvumilia ucheleweshai huu kwa muda mrefu 
kiasi hiki na zamani sana angekwisha achana na mimi. Lakini sio 
Fidahusein bhai. Kukumbusha kwake kwa mara kwa mara lakini 
kwa upole kumeleta faida. Allah amlipe malipo mema na ampe 
maisha marefu yenye siha ili aendelee kuhudumia katika njia Yake.
Yote yamesemwa na kufanywa, nimefanya hadhari kubwa kuondoa 
makosa ya aina yoyote, kiukweli au vinginevyo, kutoka kwenye kazi 
hii. Hata hivyo, kama kuna kosa la aina yoyote ile, zito au jepesi, 
Naomba msamaha wa Allah.
Mohamed Raza Mohamed Husein Dungersi, Ph.D.
New York, Marekanu
6 Juni 2010
22 Jamdiul-Thani 1431
NYONGEZA
Kabla  ya  kuchapishwa  kwa  kijitabu  hiki,  Haji  Fidahusein  bhai 
Hameer alifariki dunia mwezi Februari 6 2011.
Faraja yangu pekee ni kwamba niliweza kumkabidhi muswada wa 
kijitabu hiki wakati wa uhai wake na aliondoka ulimwenguni hapa 
akijua kwamba kazi hii imekamilika. Allah aipumzishe roho ya 
Marhum katika ujirani wa Masoomeen wetu 14.
Februari 1, 2012
1 Rabiul Awwal 1433
New York, Marekani
3
IMAM MUHAMMAD BIN 
HASAN AL-MAHDI (A.S.)
UTANGULIZI
“Na usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi  
Mungu  kuwa  wamekufa,  bali  wako  hai  mbele  ya  Mola  wao  
wanaruzukiwa.” (3:169)
Maimam  wote  wateule  kutoka  kizazi  cha  Mtukufu  Mtume  
(s.a.w.w.) (ambao kuhusu maisha yao tayari tumekwisha yajadili 
kwenye vijitabu vilivyotangulia) waliuliwa katika huduma ya njia 
ya Allah. Imam Ali (a.s.) aliuliwa wakati akiwa anasali swala ya  
alFajr katika msikiti wa Kufa. Kichwa cha Imam Husayn (a.s.)  
kilikatwa akiwa kwenye sajda katika uwanja wa mapambano wa 
Karbala. Maimam (a.s.) wengine tisa waliobakia wote waliuliwa 
kwa sumu, hivyo, maisha yao ya kimwili yaliishia katika njia isiyo 
ya kawaida. Kwa hiyo wote walikuwa mashahidi. Kwa mujibu wa 
aya ya Qur’an iliyonukuliwa mwanzoni, Maimam wote, katika hali 
ambayo sisi hatuitambui, wako hai na wanapokea riziki yao kutoka  
kwenye neema za Allah. Imam wa 12 na wa mwisho, Hadhrat  
Muhammad bin Hasan Askari (a.s.), anayejulikana kama Imam 
Mahdi, bado hajafariki kimwili. Yeye ni Imam wa zama - Al-Hujjah 
(Dhihirisho/Thibitisho), Al-Qaim (Mwazilishi) - hivi sasa kwa amri 
ya Allah, yuko katika “Ghaiba” (Ghaibu) na hafikiwi na waumini 
ingawa yeye anatambua hali ya kila mfuasi, kwa uwezo aliojaaliwa  
na Allah. Kwa amri ya Allah atajitokeza tena na kusimamisha  
utawala wa Allah katika ardhi hii kabla ya kuja kwa Qiyamat (Siku 
ya Hukumu).
Kwa Waislamu kwa ujumla, na hususan kwa Mashia, ni muhimu 
kwamba wote wanapata taarifa za msingi kuhusu Hadhrat Mahdi,  
Allah  amlinde  katika  kipindi  hiki  cha  Ghaibu,  na  aharakishe  
kujitokeza  kwake  tena.  Hii  ni  kwa  sababu  Mtukufu  Mtume  
(s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye atakufa na hamjui Imam wake 
wa zama zake, anakufa kifo cha mjinga (JAHIL).” Wanachuoni  
4
wanatafsri ‘ujinga’ kuwa na maana kutokuwa na ujuzi kuhusu mizizi 
na msingi ya Uislamu. Kwa maneno mengine, maana ya hadithi ni 
‘yule anayekufa bila kupata taarifa ya msingi kuhusu Imam mteule 
wa zama zake, anakufa kifo cha asiye Mwislamu.’
Kwa mukhtasari, taarifa kuhusu Imam wetu wa zama, Hadhrat 
Mahdi (a.s.), zinaweza kuwekwa katika vigawanyo viwili: taarifa  
ya awali na ya pili. Taarifa ya awali hujumuisha ujuzi kuhusu hai-
ba yake, kuwepo, matendo na kujitokeza kwa mara ya mwisho 
kwa Imam (a.s.). Kutokana na mwanga huu, tunahitaji kutambua  
majukumu yetu na wajibu wetu kwa Imam wakati yuko ghaibat 
yake. Kwa upande mwingine, taarifa ifuatiayo - ya pili inahusisha  
masuala  kama  makazi  ya  sasa  ya  Imam,  alipo,  dalili  ambazo  
zitajitokeza kabla ya kujitokeza tena nk. Taarifa hii ni muhimu  
kuijua, lakini sio ya muhimu sana kama taarifa zilizopo chini ya 
kigawanyo cha awali.
Katika kitengo hiki, mkazo itakuwa juu ya vigawanyo vyote - cha 
awali na kifutacho - cha pili kuhusu ujuzi wa kumuelewa Imam wa 
12, Hadhrat Mahdi, Allah amlinde katika kipindi hiki cha ghaibu, 
na aharakishe kujitokeza kwake tena. Msisitizo utakuwa pia juu ya 
jukumu la “Marjah” (wale ambao wako katika kipindi cha Ghaiba 
ya Imam (a.s.)).
5
SURA YA KWANZA
IMAM MUHAMMAD BIN HASAN (A.S.) AL-MAHDI:
KUZALIWA KWAKE NA MAISHA YA UTOTO
UTANGULIZI
Dhana ya “Umahidi” (Umasihi), au ujio wa mkombozi katika siku 
za mwisho za kuwepo kwa uhai katika ardhi hii kama tuijuavyo, 
sio uzushi wa baadae uliobuniwa na Mashia waliposwagwa mpaka  
kufikia kiwango cha hofu ya kutisha katika sura ya ukandamizaji  
kutoka  kwa  maadui  zao.  Kwani  Mtume  (s.a.w.w.)  aliwaambia 
Waislamu  katika  mzunguko  wake  katika  nyakati  mbalimbali  
kuhusu kuja kwa Mahdi. Wanachuoni mashuhuri wa Sunni na 
Shia, wakati wote wamethibitisha hili katika vyanzo vyao maarufu.  
Kwa  mfano,  Shaykhul  Islam,  Shaykh  Suleiman  bin  Ibrahim  
Al-Qunduzi Al-Hanafi anaandika katika kitabu chake Yanabi ul 
Mawaddah kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anajadiliana na 
Myahudi akiitwa Naathaal, alimtangaza Ali bin Abi Talib (a.s.) 
kama mrithi wake, ambaye baadae atarithiwa na mwanawe Hasan 
(a.s.) na kisha Husayn (a.s.). Kisha Mtume (s.a.w.w.) alimuambia  
yule  Myahudi  kwamba  mlolongo  wa  kurithi  utaendelezwa  
kupitia Maimam tisa, wote wakiwa ni kizazi cha Imam Husayn (a.s.). 
Yule Myahudi akataka kujua majina ya watoto hawa tisa. Mtume 
(s.a.w.w.) akawataja kama ifuatavyo: “Baada ya Husayn atakuwa 
mwanawe Ali bin Husayn, baada yake mwanawe Muhammad bin 
Ali, baada yake Jafar bin Muhammad, kisha Musa bin Jafar, kisha 
Ali bin Musa, kisha Muhammad bin Ali, kisha Ali bin Muhammad, 
kisha Hasan bin Ali na baada yake ni mwanawe Muhammad bin 
Hasan Al-Mahdi.” 
Tena  Shaykh  Suleiman  anasimulia  katika  kitabu  hicho  hicho  
kwamba Sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) Jabir bin Samara alimsikia 
Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Uislamu utabakia maadamu warithi 
wangu 12 wanabakia, na wote watakuwa wanatokana na Kureish.” 
Bukhari, Muslim na Tirmidh wanasimulia hadithi kama hiyo hiyo 
kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.).
6
Description:ya usimamizi wa karibu wa Allama Rizvi, ambaye mwongozo wake  Mtaje Imam (a.s.) kupitia Ziyarat maalumu zilizopendekezwa kwa ajili ya