Table Of Content[COMPANY NAME]
[Company address]
1
Isaack Nsumba
Toleo la kwanza June, 2021
@Haki zote zimehifadhiwa, hairuhusiwi kutoa
sehemu yoyote ya kitabu hiki bila ruhusa ya
mwandishi.
Hatua
kali
za
kisheria
zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote, taasisi au
shirika lolote lile litakalodiriki kufanya hivyo.
Isaack & Rebecca Nsumba
P.O. BOX 674, Dodoma-Tanzania
Phone: +255654722733
+255672356147
THE ARTS OF GIVING AND RECEIVING
GIFTS IN RELATIONSHIP
2
SHUKRANI
Ninamshukuru
Mungu
kwa
namna
alivyonifanya niwe mtu mwenye kugusa
maisha ya wengi kupitia makala, vitabu na
semina
mbalimbali
ambazo
nimekuwa
nikifanya kwa msaada wake, ninawashukuru
wote ambao Mungu amekuwa akiwatumia
katika namna ya moja kwa moja au isiyo na
moja kwa moja kuhakikisha ile kiu iliyo ndani
yangu
ya
kuona
mabadiliko
yanatokea
kwenye maisha ya watu hasa kwenye eneo la
ndoa na uchumi, ninamshukuru mpenzi
wangu
Rebecca
kwa
namna
ambavyo
amekuwa akinitia moyo na kuonesha kuamini
pamoja nami katika kitu ambacho mungu
ameweka ndani yangu kwaajili ya dunia.
3
YALIYOMO
SHUKRANI ........................................................................... 2
YALIYOMO ........................................................................... 3
UTANGULIZI ........................................................................ 4
SURA YA KWANZA ............................................................... 7
SANAA YA UTOAJI ................................................................ 7
AINA ZA ZAWADI ................................................................... 9
UMUHIMU WA ZAWADI KATIKA KUKUZA, KUIMARISHA NA
KUSITAWISHA MAHUSIANO. .............................................. 20
MAKOSA YA KUEPUKA WAKATI WA KUCHAGUA ZAWADI
YA KUMPELEKEA MWENZI WAKO ...................................... 26
SURA YA PILI ..................................................................... 31
SANAA YA UPOKEAJI .......................................................... 31
DHUMUNI LA KUTOA .......................................................... 33
UMUHIMU WA KUTOA SHUKRANI KAMA ISHARA YA
KUPOKEA ............................................................................. 36
NAMNA YA KUSHUKURU .................................................... 44
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI UNATOA SHUKRANI
KAMA ISHARA YA KUPOKEA HUDUMA .............................. 48
KUHUSU MWANDISHI ......................................................... 51
4
UTANGULIZI
Kipekee kabisa mimi pamoja na Mpenzi
wangu Rebecca tunasema ahsante kwa wote
ambao kwa namna moja ama nyingine
wamekuwa
msaada
katika
kuhakikisha
tunaifikia hatma ya wito wetu tuliopewa na
Mungu hapa duniani, tunatambua mchango
wa kila mmoja iwe ni wa kifedha, kimawazo
na hata wa kimaombi pia katika kuhakikisha
tunawafikia watu wengi zaidi kupitia maarifa
ambayo tumekuwa tukitoa kwenye mitandao
ya kijamii, makanisani pamoja na kwenye
makala mbalimbali na vitabu kama hiki. Ni
matumaini yetu kuwa, kila atakaebahatika
kusoma
kitabu
hiki
hali
ya
hewa
ya
mahusiano yake itabadilika hasa kwenye
eneo la kutoa na kupokea zawadi.
Yamkimnin umekuwa ukitoa huduma Fulani
kwa mwenzi wako lakini bado unaonekana
kama hauugusi moyo wake sawasawa na vile
5
yeye anavyotaka au mwenzi wako amekuwa
akijitahidi sana kutoa huduma Fulani huku
akitegemea aina Fulani ya upokeaji na
muitikio
kutoka
kwako
lakini
namna
unavyoitikia inamvunja moyo na kumkatisha
tamaa, kitabu hiki kimelenga kuwasaidia
wapenzi wote kuboresha mahusiano yao
kupitia kitgendo cha kutoa na kupokea iwe ni
zawadi au aina Fulani ya huduma, ni kitabu
ambacho kinalenga kuimarisha ngazi zote za
mahusiano yawe ya kindugu, kikazi, kirafiki
au ya kimapenzi (uchumba na ndoa) kwenye
eneo la kujua namna ya kupokea vitu kutoka
kwa watu.
Usipojua namna ya kupokea unaweza jikuta
unajifungia mlango wa kupokea vitu vingi
hata Kama unastahiri kupokea, lakini pia
ukiwa hujui namna ya kutoa katika namna
inayomgusa uliemkusudia unaweza jikuta
huduma yako inageuka kuwa kero
na
kupelekea mgogoro kati yako na mwenzi
wako.
6
Ni kweli kwamba wahenga walisema “tenda
wema (saidia, toa zawadi) ila usingoje
shukrani”, kauli hii haimaanishi kuwa kwa
sababu
huwa
hatungoji
shukrani
basi
hatuhitaji kupokea shukrani kutoka kwa watu
tuliowatendea mambo mazuri; isingekuwa
rahisi
kwa
wahenga
kusema
“usingoje
shukrani” ikiwa wanajua wazi kuwa hatuhitaji
kushukuriwa, kauli hiyo inaashiria kuwa hitaji
la msingi la kihisia la kila mwanadamu ni
kujua jinsi kitu alichokifanya kwa mtu
mwingine hasa ikiwa ni kizuri kilivyougusa
moyo wake na hisia kwa ujumla.
7
SURA YA KWANZA
SANAA YA UTOAJI
MAANA YA ZAWADI, AINA NA UMUHIMU
WAKE
Tunapozungumzia
kuhusu
“zawadi”
tunaznungumzia kitendo cha kuelezea hisia
zako za upendo kwa mtu mwingine kupitia
vitu, zawadi ni ishara, kiashiria au kielelezo
cha thamani ya mpokeaji au nafasi aliyonayo
mpokeaji ndani ya moyo wa mtoa zawadi.
Watu wengi kwa kutokujua nguvu iliyojificha
ndani ya zawadi wamekuwa wakilichukulia
jambo
hilo
kiwepesi
bila
kulipa
uzito
unaotakiwa,
lengo
la
kitabu
hiki
ni
kukupandikizia
ufahamu
utakaokusaidia
kulichukulia suala la zawadi katika namna ya
uzito unaotakiwa na jinsi unavyoweza kuwa
mbunifu katika kuchagua aina ya zawadi
inayoendana na kile unachotaka mwenzi
wako ajue baada ya kupokea zawadi yako.
8
Lengo
la
kutoa
zawadi
ni
kufanya
mawasiliano kati ya mioyo yenu miwili au
kuwasilisha aina Fulani ya hisia kwa mwenzi
wako (the primary purpose of giving a gift is
to communicate your feelings to your
spouse). Ndani ya zawadi yoyote ile kuna
ujumbe umebebwa na mpokeaji itakuwa
rahisi kuupokea bila hata mtoaji kufungua
kinywa chake na kusema, hivyo itakuhitaji
ubunifu wa hali ya juu zaidi ili ujumbe
utakaopokelewa
na
mpokeaji
baada
ya
kumpatia
zawadi
uendane
na
kile
ulichokusudia.
kama suala la utoaji lisipofanyika kwa
umakini na kwa ubunifu mkubwa basi zawadi
inaweza ikatumika kupeleka aina ya ujumbe
ambao haukukusudiwa na mtoaji wa zawadi.
9
AINA ZA ZAWADI
Katika kuangalia aina za zawadi ni muhimu
kwanza tuchunguze aina za upendo, kwani
kupitia hizo ndipo tutaweza kubaini aina za
zawadi
kwa
sababu
aina
ya
zawadi
inasukumwa na aina Fulani ya upendo, yaani
zawadi ni alama inayosimama kuwakilisha
aina
Fulani
ya
mahusiano
ambayo
yamejengwa juu ya aina Fulani ya upendo.
1. UPENDO WA AGAPE - UPENDO WA
MUNGU. (Godly Love)
Agape ni aina ya upendo wa ki-Mungu,
utendao kazi ndani ya mtu pasipo masharti
yoyote
au
sababu
yoyote.
Ni
upendo
usioangalia hali ya nje ya mtu. Ni nguvu au
uwezo wa mvuto wa Ki-Mungu utendao kazi
ndani ya mtu, kumwonyesha mtu mwingine
wema wa Mungu bila kujali hali yake yoyote.
Ni
upendo
usio
na
sababu
yoyote;
unampenda mtu kwasababu tu unatakiwa
kumpenda, nukta. Hakuna sababu nyingine.
10
Kwa kingereza wanasema “unconditional
love”.
Aina hii ya upendo; agape, ni kama ule
aliotuonyesha Mungu kwa kutupenda. Neno
la Mungu linasema ‘Mungu alitupenda tungali
wenye dhambi’, yaani bado tuna dhambi,
madhaifu na bado akatupenda (Rum 5:8) ili
atuokoe na mauti itokanayo na uasi kwa
Mungu. Imeandikwa katika biblia kwamba
Mungu aliupenda ulimwengu wenye kila aina
ya uovu, uasi na uchafu (Yoh 3:16, Rum 1:28-
32) na akamtoa Kristo afe kwa ajili yetu, ili
tuokolewe. Kwahiyo, alitupenda bila kujali
uchafu na uasi tuliokuwa nao. Huo ndio
upendo wa agape.
Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa ki-Mungu
(Agape).
i. Hauangalii hali ya mtu ya nje.
ii. Hauna masharti yoyote ya kupenda.
iii. Hauna kipimo au kiwango cha kupenda.
iv. Hauna mwisho au kikomo cha
kupenda.
11
2. UPENDO
PHILEO
–
UPENDO
WA
KIRAFIKI. (Friendship Love)
Phileo ni upendo wa kirafiki. Huu ni upendo
wa tofauti kidogo na upendo wa agape.
Phileo ni upendo wenye sababu. Kiingereza
wanasema ‘conditional love’. Ni upendo
wenye
sababu.
Huu
ndio
upendo
unaokuwepo kati ya marafiki. Phileo ni
upendo unaoshikiliwa na kishikizo/kifungo
cha ‘masharti’ fulani au ‘sababu’ fulani. Mtu
huwa rafiki wa mtu fulani ‘kwasababu’ fulani.
Kuna mazingra yamewafanya watu fulani
kuwa marafiki. Mazingira hayo au masharti
fulani yakivunjika kati yao, basi upendo ulio
kati yao huyeyuka na urafiki wao huvunjika.
Aina hii ya upendo wa phileo ni kama ile
ambayo Yesu anaisema katika kitabu cha
Yohana 14:21,23. Anasema kwamba ‘mtu
akinipenda, Baba atampenda, nami na Baba
tutakuja kufanya makao ndani yake’. Huu ni
upendo tofauti na ule unaotajwa katika
Yohana 3:16 na Warumi 5:8 ambao unasema
12
Mungu alitupenda tungali wenye dhambi
pasipo masharti yoyote. Yaani, kwa upendo
agape, Mungu hakujali hali zetu za nje wala
masharti yoyote. Lakini kwa upendo phileo,
Mungu
anaangalia
kwanza
kama
mtu
atatimiza masharti aliyoyaweka, kisha ndipo
na yeye Mungu anaachilia upendo phileo kwa
mtu huyo, anakuwa rafiki yake. Mahali
pengine Yesu alisema kwa wanafunzi wake
kuwa ‘siwaiti ninyi tena watumwa bali
marafiki.’ Hilo neno ‘tena’ linamaanisha
kwamba, baada ya kukaa na wanafunzi wake
kwa muda fulani, waliweza kufikia kiwango
Fulani cha masharti alichokitaka Bwana, hata
sasa wamefika katika ngazi wa kuwa marafiki
wa Yesu na sio watumwa tena. Ndio maana
imeandikwa pia katika kitabu cha Mithali 8:17
kuwa, ‘ninawapenda wale wanipendao …’
Hivyo phileo ni upendo wenye masharti na
sababu. Rafiki wa mtu husema ‘nampenda
mtu Fulani, rafiki yangu kwasababu…’ Labda
kwa sababu wanasoma wote au kwasababu
13
alimsaidia katika eneo fulani au kwasababu
anatabia fulani au kwasababu wanatoka kijiji
kimoja, n.k.
Sifa kuu tatu (3) za Upendo wa kirafiki
(Phileo).
i.
Unaangalii hali ya mtu ya nje.
ii.
Una
masharti
yoyote
ya
kupenda.
iii.
Una kiwango au kipimo cha
kupenda.
iv.
Una mwisho au kikomo cha
kupenda.
3. UPENDO
STORGE–
UPENDO
WA
KIFAMILIA. (Family Love)
Upendo storge ni upendo wa kifamilia, ni
upendo unaotokana na damu moja ya
undugu. Ndugu wa damu moja hata kama
hawapatani au wemegombana, bado ndani
yao kuna upendo wa kindugu. Fikiria; mtu na
mdogo wake wakiwa wamegombana sana na
14
kutupiana mito ya makochi na vitabu vyote
vya kwenye shelfu za kabati, baadaye, mmoja
akimkuta
ndugu
yake
anaonewa
au
anagombana
au
anapigwa
na
muuza
machungwa wa mtaani, huyu ndugu yake
kwa vyovyote ataguswa tu, ataonyesha kujali
tu au anaweza hata kuweka tofauti zao
pembeni na kuingilia kumsaidia. Msukumo
huo au mvuto huo, ni mvuto unaotokana na
viini
vya
upendo
wa
kifamilia
unaowafungamanisha watu wa damu ya
familia moja au ukoo mmoja.
Upendo wa kindugu, storge unafanana kwa
sehemu na ule upendo wa ki-Mungu wa
agape.
i. Hauangalii hali ya nje ya mtu.
ii. Hauna masharti ya kupendwa.
iii. Hauna kikomo au mwisho wa kupendwa.
Tofauti yake moja kubwa na upendo wa
agape ni kwamba, upendo wa kindugu una
kiwango au kipimo cho kupenda. Ndugu
wanapendana lakini kwa viwango tofauti;