Table Of ContentJQ 3515
.T164
TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION
MAISHA YA UJAMAA
see
C
h
o
INGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION
MAISHA YA UJAMAA
Bei 1/50
Tanganyika Ifrican National Ilsvos .
MAISHA YA UJAMAA
J Q 3515
.T 164
INDIANA UNIVERSITY
LIBRARIES
BLOOMINGTON
Makao Makuu ya TANU
Dar es Salaam
21
N
Y
4-3.75
MAISHA YA UJAMAA
Ili tuwe wajamaa halisi hatuna budi tuishi kljamaa;
hakuna anayeweza kuwa mjamaa, na huku anaishi
maisha ya peke yake. Kuishi kijamaa ni kukaa pamoja
na wengine, na kufanya kazi pamoja, kwa manufaa ya
wote. Kuishi na kufanya kazi pamoja si jambo rahisi,
hasa katika siku za mwanzo, ingawa sababu za kuishi
katika kijiji cha ujamaa ni rahisi kuzieleza. Watu wengi
wanaoishi pamoja kwa kuheshimiana na kwa mpango
.
maalum wa kazi wana nguvu zaidi kuliko mtu pekee.
lli juhudi ya kuishi na kufanya kazi pamoja ifanikiwe,
lazima wote wanaohusika wazielewe tokea mwanzo
shabaha zao, na wawe na shauku ya kuzitimiza. Jambo
1
1
muhimu sana litakalofanya vijiji vya ujamaa viendelee ni
wanakijiji wenyewe kuelewa shabaha zao, na kuwa na
ujuzi wa kuzitekeleza.
Kusema kweli kile kitendo cha watu waliokuwa
maskini na wasio na elimu kukusanyika pamoja haki
wafanyi wawe wakulima matajiri zaidi, na wenye ujuzi
Bali kitendo hicho cha kukusanyika pamoja
bora.
huwapa uwezekano wa kufanya kazi zaidi katika juhudi
zao za kupambana na Umaskini na Ujinga.
Ni wajibu wa TANU na Serikali kufanya kila juhudi
ya kuwaeleza watu kuwa mipango ya kuishi pamoja
huleta maisha bora zaidi. Na haitoshi kuwaeleza tu, bali
pia kuwaonyesha kwa mifano iliyo wazi jinsi faida hizo
zitakavyopatikana. Lakini kwa vyo vyote vile ni juhudi za
wanakijiji wenyewe tu zinazoweza kuyatimiza yale
yanayoweza kutendeka.
Hapana sababu ya kuanzisha au kujiunga na kijiji
cha ujamaa ila kwa nia ya kutaka kuleta mabadiliko, au
mapinduzi. Mapinduzi yo yote ni ya mtu binafsi, hakuna
1
anayeweza kumfanyizia mwenziwe mapinduzi. Vijiji vya
Ujamaa ni vya wale waliochoshwa na umaskini, na
kukasirishwa na ujinga na maradhi. Vijiji vya Ujamaa
ni kwa wanaume, wanawake na watoto, walio na hamu
ya maisha mapya, wakitambua kuwa maisha hayo
mapya hayawezi kujengeka isipokuwa kwa kugeuza
kabisa maisha ya zamani, na sasa wako tayari kufanya
kazi kutwa kucha ili kujiondosha katika hali yao ya
unyonge.
Watu wanaoishi katika Kibutzi, yaani vijiji vya
ujamaa vya huko Israeli, au katika 'Kommune', yaani
vijiji vya Ushirika huko China, walifanya kazi kwa juhudi
kama hiyo, na wakagundua kuwa matokeo yake
yalikuwa ni ya kuridhisha sana. Kuanzisha kijiji cha
Ujamaa ni kuanzisha vita, kupigana na Umaskini, Ujinga
na Maradhi. Ili kushinda umaskini, ujinga na maradhi
wanakijiji hawana budi kupigana vita vikali. Kama watu
katika kijiji cha Ujamaa hawakushirikiana kijeshi katika
juhudi zao, wakitumia akili na taratibu nzuri, wasitu
maini kushinda katika vita hivi. Wakazi wa kila kijiji cha
Ujamaa lazima wawe jeshi la watu linalopigana vita vya
watu; vita vya kutafuta amani na maisha bora. Ni vita
vikali, na ili kushinda katika vita hivyo unahitajiwa
ushujaa na juhudi nyingi. Wanaoweza kujenga vijiji vya
Ujamaa ni watu wale wanaoamini mipango ya kijamaa,
na kujitolea kujenga maisha ya kijamaa kwa faida ya
watu wote.
Maneno haya, kujitolea, kuelewa, kujua, kushiri
kiana, kuwa na hakika, utaratibu wa kazi, ushujaa,
juhudi, utundu, ni maneno mazuri; lakini yana maana
gani? Yana maana gani kwa kazi za watu wanaoishi
katika kijiji cha Ujamaa, siku baada ya siku, mwezi
baada ya mwezi, mwaka baada ya mwaka, ili kujipatia
riziki na maisha bora? Yana maana gani kwa wazee
waliokwisha fanya kazi maisha yao yote; kwa wanaume,
wanawake, watoto; kwa vijana wenye afya na ari, na
2
wasichana? Yana maana gani kwa ardhi, nyumba,
majembe, mpunga, mbegu, jua kali, mahindi, pamba,
kahawa, ng'ombe, mbuzi na kuku? Maswali haya haya
wezi kujibiwa ila kwa vitendo. Tutayaeleza maneno
hayo, ili tujiandae kwa vitendo.
UMOJA
Umoja huzaa nguvu. Umoja ni nguvu; utengano ni
udhaifu. Haya ndiyo maneno yaliyotuongoza katika
kupigania Uhuru! Mpaka sasa yangali na maana. Ingefaa
kila kijiji cha Ujamaa kuyaandika maneno haya kwa
herufi kubwa katika ukumbi wa mkutano. Umoja ndio
msingi mkuu wa maisha ya kijiji cha Ujamaa. Lakini
umoja huu unaweza kujengwa, kuhifadhiwa na kudu
mishwa namna gani? Umoja unategemea watu
kuelewana, kuheshimiana na kuaminiana. Wale watu
wanaoanza kijiji cha Ujamaa lazima wajuane vema, na
lazima wajadili kiasi cha kutosha kitu cho chote wana
chotaka kufanya, ili waweze kkuuaammiinniiaannaa.. Lazima
waelewe wazi kwamba:
1 . Juhudi tunazofanya pamoja ni zetu wote,
kwa hivyo wajibu ni wetu wote.
Wajibu wa kwanza uwe kati yao wenyewe,
2.
wala siyo kwa ndugu walio nje ya kijiji.
3. Wote wako tayari kufanya kazi kwa bidii na
kuvumilia hata wakati wa shida kubwa.
Mtu mvivu, yule anayedharau madaraka yake,
mlevi, au mgomvi, hawa wote si rahisi kuwa nao katika
.
kijiji cha Ujamaa. Ikiwa mtu ana walakini katika tabia H
yake, itafaa wakazi wa kijiji cha Ujamaa wafikirie sana
kabla ya kumkaribisha kuishi nao, na hata wakimka
ribisha lazima wawe na utaratibu mzuri wa kumchunga,
na kama lazima wawe na muda wa kuchunguza tabia
yake kabla hajakubaliwa. Vijiji vingi vya Ujamaa
3
N
anayeweza kumfanyizia mwenziwe mapinduzi. Vijiji vya
Ujamaa ni vya wale waliochoshwa na umaskini, na
kukasirishwa na ujinga na maradhi. Vijiji vya Ujamaa
ni kwa wanaume, wanawake na watoto, walio nahamu